6 Points To Note When Giving Testimonies
1. Kabla hujaanza,
piga sala- Pray before you begin. Kuomba ni
kuzungumza na Mungu, kabala hujafanya chochote, mhusishe yeye Muumba wa vyote.
2. Eleza shida/dhambi
yako- Talk your sin. Wafanye wanaokusikiliza ama kukutazama
waelewe ni kwa nini uliamua upande wa Bwana. Usiorodheshe dhambi zako, hapana,
zungumza kitu cha maana kilichofanya ukaamini uwepo wa Mungu.
3. Ongelea suluhu-
Talk of the solution. Ukishaeleza dhambi zako
na kilichokuvutia kwa Mola, waambie wasikilizaji wako baada ya kumjua Mungu,
uliipata suluhu gani na kiaje. Ni muhimu sana ili kuwavutia wasiomjua Mungu na
pia wale ambao wako na shida na dhambi kama zako.
3. Sema ukweli- Be
honest. Usitoe ushuhuda ili kumfurahisha mtu. Sema maneno
ya ukweli ambayo umeyashuhudia mwenyewe. Kuna watu ambao wanapenda tu waonekane
mbele ya watu wakiongea lakini wanachokizungumza ni upuzi mtupu. Kama huna
uhakika na jambo lolote, liepuke kuliongelea mbele ya uma sababu utawapotosha.
Kuwa mkweli.
4. Toa mifano bora-
Give relevant examples and stay focused. Wakati wa
kutoa ushuhuda, ni muhimu sana utumie mifano. Lakini usitoe bora mifano sababu
nimesema utumie mifano, toa mifano bora na inayo ambatana na unachokizungumzia.
Pia usiende nje ya mada yako, usiwapotoshe kondoo.
5. Usitumie maneno
magumu- Avoid vocabularies. Msikilizaji na
mtazamaji huenda sio wa haiba au ngazi yako kimasomo, huenda unayaelewa maneno
mazito mazito na ya ndani ya Bibilia ama Koran lakini yeye haelewi. Kwa sababu
hii, tumia lugha na maneno mepesi ambayo kila mtu, ndio kila mtu, atakuelewa
bila kumpa kibarua.
6. Chunga wakati-
Watch your time. Hakuna kitu ambacho huchosha watu kama
kuutumia muda wao zaidi ya mlivyoelewana. Hakikisha unautumia muda uliotengewa
na ikiwezekana jaribu kupunguza kidogo ili usiwaudhi, usiwabore, watu.
Ukipitisha muda, ole wako, hawatukusikia tena. #ASANTE

I really like this, inapendeza sana. God Bless!
ReplyDelete