1. Mtu wa kwanza kufikiria- The first person you think of. Kama kila siku ukirauka asubuhi mtu fulani ndio wa kwanza
kuwaza, basi jua kwamba kuna msukumo wa kimapenzi baina yenu. Mtu huyu
ukifikiria kumhusu pia unabambika tu na kujawa na raha.
2. Kipaumbele- You prioritize the person first. Kabla ya wewe kuingiwa na hisia za kimapenzi/mahaba, ulikuwa
unajipa kipaumbele. Yani ulijiona mtu bora kabisa katika sayari na mambo yako
ulitaka kuyatimiza kabla ya wengine lakini ukiona ushaanza kupatia kipaumbele
mambo ya mtu mwingine, jua basi hayo ni mapenzi. Ushaanza kuogelea katika
bahari la kimahaba.
3. Utafanya Chochote- You will do anything. Ikiwa mtu ambaye mko katika uhusiano naye huwa unamfanyia ama
uko tayari kumfanyia chochote ili kumridhisha, na yeye pia atafanya lolote kwa
ajili yako, basi bila shaka hapo kuna mapenzi.
4. Hakuna
haya/aibu – You aren’t embarrassed when together.
Kama ‘mtu wako’ hamhaibiki wakati mko pamoja, basi hayo ni mapenzi sababu kuna
mtu ambaye mkiwa naye hata barabarani hutaki akushike mkono sababu labda havai
vizuri, sio mrembo/mtanashati yani hana beauty yoyote. Kama mnatambulishana
hata hadharani kwa marafiki, dah! mahaba niue.
5. Tabia
unazopenda- Qualities you prefer. Kama
mwenzako ako labda na zile tabia unazotamani mpenzi wako awe nazo na kila saa
ukimwambia anaona kama unamtania, basi jua huyo ndiye. Yaani unaona hakuna
mwingine isipokuwa yeye tu! Raha kweli kweli chambilecho Ali Kauleni.
6. Fikra
kubwa/ You think big. Ukitaka kujua kabisa kama unaogelea
katika bahari la mapenzi, kila mara ukiwaza kuhusu mpenzi wako unaona tu mambo
makubwa. Unaanza kupanga akilini jinsi mtakavyo ishi pamoja, wapi mtaishi,
nyumba mtaishi, familia kiasi gani NK. Hapo ni mahaba tupu aisee.
7. Mpenzi
ni rafiki wa karibu- The person is your closest and best friend.
Kama mpenzi wako ndiye rafiki wa karibu kabisa na hakuna siri kubwa kubwa baina
yenu, basi huyo ndiye mpenzi. Hisia zako kwake hazina kipimo wala masharti. Wapenzi
ni marafiki yani kufa kuzikana. #ASANTE

Walahi Kakamusa utatumaliza,,, great tips man.
ReplyDelete