Monday, 22 February 2016

HOW TO DEAL WITH MONDAY BLUES, UTAPENDA.....

                      Njia Nne Za Kuhepa Monday Blues...

           

1.Tengeneza mazingira mapya- Build an Inner World. Unapohisi umelemewa kabisa ama umeboeka sana, jaribu kutafuta mazingira mapya. Si maanishi uumbe ulimwengu wako, ah ah! Namaanisha ujaribu kutafuta mahali tofauti na ulipo wakati umeboeka. Mazingira mapya katika fikra zako yatasaidia kulipa deni akilini mwako deni ambalo linachangia kuboeka. Tafuta idea mpya na tofauti.

2. Fanya jambo la dhamana na maana- Seek Quality. Je unachokifanya sasa hivi ni nini? Kinadhamana au maana yoyote? Ni kitu gani ambacho ni cha dhamana ndani yako? Dhamana ndio kitu cha muhimu maishani. Wakati umeboeka hakikisha unajiuliza haya maswali na ukishayajibu, utaondoa kuboeka ndani yako.

3. Kubali hali kisha pambana- Accept the situation then resist. Huenda una kazi nyingi sana ya kufanya, uko busy. Kubali hali ilivyo alafu tafuta mbinu za kijanja za kupambana na hali ya kuboeka. Unaeza ukapumzika kwa dakika kadhaa, break, kunywa kinywaji ukipendacho lakini sijasema kileo, nhaha.

4. Jifungue minyororo- Unchain yourself. Uhuru wa akili ni kitu muhimu sana katika hii sayari ya pekee yenye uhai, Dunia. Usiwe mtumwa wa kazi ambayo unaifanya, usijilazimishe katika chochote. Taratibu tu kama taarab na mambo yatakuwa laini kama mstari. #ASANTE.

1 comment: