Monday, 29 February 2016

LAST MINUTE INTERVIEW? THIS IS HOW TO PREPARE...

 Njia Tano Za Kijiandaa Kwa Interview...
1. Fanya utafiti- Conduct a Research. Kama umeitwa interview na haukuwa umejiandaa ama umearifiwa kwa kuchelewa, labda umeambiwa ni kesho ama ni ya jioni, hakikisha umefanya utafiti hata kama kiasi tu kuhusu kazi yenyewe, kampuni na ni nini kinachohitajika.
2. Panga stakabadhi zako- Arrange your papers/Docments well. Sababu uko na masaa machache to ndio uende hiyo interview, zipange karatasi zako vizuri na ziwe nadhifu.
3. Andaa historia/hadithi fupi kukuhusu- Prepare and memorize your story. Hakikisha unaweza jieleza na kueleza vile unaweza fanikisha ikiwa utapata hiyo nafasi. Jiandae ama ubuni vipi utaweza kujieleza. Muhimu sana, jiulize wewe ni nani?
4. Utavaa nini na aje? What will you wear? Ni nguo gani utavalia katika hiyo interview? Utaivaa aje? Hapa pia inategemea interview ni ya nini na muktadha wake. Kama ni kazi ya ofisi tafuta suti, hakikisha unaivaa, isikuvae, nhaha, piga pasi na utakuwa nadhifu/smart.
5. Wakati- Keep time. Usichelewe hata kidogo kufika katika ukumbi/Venue wa interview yenyewe. Fika kabla ya wakati tafadhali rafiki yangu. #ASANTE

No comments:

Post a Comment