Friday, 19 February 2016

HOW TO MAINTAIN YOUR FRIEND(S)


  5 STEPS THAT CAN KEEP YOUR FRIENDSHIP ALIVE!!






 1. Kuwa msema kweli- Be Honest. Usiwe mtu wa kudanganya kila wakati. Uhusiano ambao umejengwa kwa uongo haudumu sababu wakati mmoja uongo utakuaibisha. Kuwa mtu wa kusema ukweli na uhusiano wenu utakuwa wa kudumu. Lakini kuna mtu aliniambia eti, kuna uongo  uonaofaa.

2. Kuwa Tayari kurekebishwa- Accept Corrections. Kuna mtu ambaye hata afanye kosa lipi, yeye anaona ako poa, hataki kukubali amekosea. Kukubali makosa sio dhambi, kubali umekosa kasha ukirekebishwa, rekebikika. Hata Bibilia husema, mwenye hapendi kurekebishwa ni mpumbavu.


3. Tenga wakati wa urafiki na ushukuru- Make time and always appreciate. Muda ndio kitu cha dhamana sana katika urafiki/uhusiano. Tenga wakati na rafiki wako/zako na mzungumze, mcheze, mcheke. Mtaniane NK. Kisha wakati wowote rafiki yako anakufanyia kitu, hakikisha umemshukuru na utaudumisha uhusiano.


4. Kuwa mjanja na usiwe mtu hivi hivi- Be wise and don’t make assumptions. Ninaposema uwe mjanja simaanishi uwe na ujanja wa ‘Nairobi’ na maanisha uwe mtu wa kuona mbele na mtu ambaye anaweza jitegemea. Usitegemee rafiki yako. Rabbit Kaka Sungura alishasema, “Mi si mtu hivi hivi”. Sawia, usiwe mtu wa kukurupuka, wakati rafiki yako hajafanya jambo fulani, usha ‘mjudge’ si poa.


5. Fanya Haki- Do right instead of being right. Unapo fanya jambo lolote, jiulize kama ni haki unachokifanya, je, inastahili? Je, unachokifanya ungependa wewe ufanyiwe? Tenda wema uende zako. Usiwe kila mara wewe ndio unaona vyako ndio haki tu!
  #ASANTE

1 comment:

  1. Natazimia mwanahabari atakayebadili jamii kupitia mfumo wa uandishi. Juhudi zako zatambuliwa Bingwa. Kazi Bora Ba mdogo.

    ReplyDelete