The following are 12 key points that can help bring back your friend..
1.Tafuta chanzo cha kukosana. Ni nini
haswa kilichozalisha uhasama na kuchangia kutoelewana kwenu. Tambua chanzo hiki
kisha ukabiliane nacho kisawasawa.
2.Usichukulie mzaha. Marafiki
ndio hupenda mzaha na kutaniana, lakini wakati unasuluhisha tatizo, weka mzaha
kando ndio muelewane.
3.Kuwa tayari kuchukua majukumu na kusamehea.
Wajibika kiutu na usahau yaliyopita, kwani ni ndwele? Toa msamaha kama
ulikosewa na kama ulikosa pia omba msamaha.
4.Fikiria utakachomwambia mwanzo na mapema. Kabla
ya kupanga lini na wapi mtakutana, jipange na lugha utakayotumia. Fikiria
maneno ya kuzungumza. Uwe mpambe wa ‘kiswahili’.
5.Mpigie simu na umuombe mkutane. Ukiwa tayari
na ‘maneno’, mpigie simu aliyekuwa rafiki yako na umuombe mkutane ili kutafuta
na kuleta suluhu ya tatizo lenu.
6.Mwandikie ujumbe, sms, ama barua. Baadhi
ya wati huwa na hasira na kisirani, huenda asishike simu yako. Wakati kama huu,
mtumie ujumbe.
7.Mwonyeshe maana ya urafiki. Urafiki
ni kama dhahabu, una dhamani kubwa. Asiye na rafiki basi duh! Sijui..
8.Sikiliza aliyonayo pia. Mkisha
kutana, usiwe unaongea peke yako, mpatie nafasi pia azungumze, ajieleze na
afungue aliyonayo. Kuwa makini.
9.Ongelea mabadiliko. Mwonyeshe
jinsi ambavyo umebadilisha tabia anazozichukia. Ongelea mambo ya kujenga.
10.Mpe muda afikirie kuhusu urafiki wenu. Baada
ya nyinyi kuzungumza, mwache rafikiyo afikirie na awaze kuhusu maelewano yenu.
11.Kuwa na subira. Usiwe na pupa. Haraka haina
baraka na pia mwenye pupa haadiriki kuvila vitamu. Vijana wa mjini wanasema, ‘kuwa
mpole’. Ukitaka heri, basi subiri.
12.Weka mipango na mikakati maalum ya urafiki. Mkishaelewana,
wenga mipango ya ni vipi mtaishi na kuudumisha urafiki wenu. Usikubali tena
urafiki uyumbe kama mawimbi ya bahari. Kuwa shupavu na ngangari. #ASANTE

Nhaha noma sana. What a great idea there, longing for more...
ReplyDeleteThanks man
DeleteGood Read,..KakaMusa
DeleteShukrani Bingwa. Mwelekeo mwema umechukua. Naomba uwe ukinitumia Barua pepe khaemba80@gmail.com kila unapochapisha bango. Asante
Delete